Courtois abakiza kutambulishwa tu - Darajani 1905

Courtois abakiza kutambulishwa tu

Share This

Chelsea imetoa taarifa kwamba imeingia makubaliano ya kumuuza mlinda mlango wake nambari moja, Thibaut Courtois kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Chelsea ilibakiza mkataba wa mwaka mmoja na mlinda mlango.huyo na kama angeendelea kubaki bila kusaini mkataba mpya basi ingemaanisha kipa huyo angeondoka bure kutokana na kumaliza mkataba wake.

Kuondoka kwa kipa huyo kunamaanisha Chelsea inafanikiwa kumnasa kwa mkopo nyota raia wa Croatia, Mateo Kovacic kama sehemu ya mabadiliko ya kipa huyo.

Mateo anatua Chelsea na huenda akatangazwa kuwa nyota wa Chelsea muda wowote kuanzia sasa kabla ya kufungwa kwa dirisha hili kubwa la usajili linalofungwa hapo kesho.

No comments:

Post a Comment