Rasmi; Chelsea yakamilisha usajili wa Kepa - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea yakamilisha usajili wa Kepa

Share This

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa mlinda mlango raia wa Hispania, Kepa Arrizabalaga akitokea klabu ya Athletic Club na kusaini mkataba wa miaka saba wa kuitumikia Chelsea

Dau la paundi milioni 71 linatajwa kukamilisha uhamisho wa mlinda mlango huyo mwenye miaka 23.

Kepa amekamilisha usajili huo ambao unamfanya kuwa mlinda mlango ghali zaidi duniani huku pia akiwa ndiye mchezaji ghali zaidi klabuni Chelsea akiipiku rekodi iliyowekwa na Alvaro Morata aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 60 akitokea klabu ya Real Madrid katika dirisha kubwa lililopita.

Kutua kwa Kepa kunafungua milango kwa Thibaut Courtois kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment