Chelsea yatamba, yaibamiza Juventus uku Aluko akirejea nyumbani - Darajani 1905

Chelsea yatamba, yaibamiza Juventus uku Aluko akirejea nyumbani

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women ambayo kabla ilikuwa ikitumia jina la Chelsea Ladies imefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 3-0 ikicheza dhidi ya klabu ya soka ya wanawake ya Juventus katika mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019.

Magoli ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na Ramona Bachmann, Maren Mjelde na Fran Kirby lakini jambo la kuvutiwa ni pale mkongwe na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea FC Women, Eniola Aluko aliporejea kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Kingsmeadow, lakini safari hii akiwa kama mchezaji wa Juventus.

Fran Kirby, Ji So-Yun na nyota wengine akiwemo Ali Riley ambaye amesajiliwa katika dirisha hili kubwa la usajili walikuwa ni sehemu ya wachezaji waliocheza mchezo huo kwa upande wa Chelsea.

Unalopaswa kulijua ni kwamba mchezo huu uliwakutanisha mabingwa yaani Chelsea FC Women akiwa bingwa wa ligi kuu nchini Uingereza (FA WSL) huku kwa Juventus wao wakiwa mabingwa wa ligi kuu ya wanawake nchini Italia, wakitwaa ubingwa huo katika msimu wao wa kwanza toka kuanzishwa kwao.

No comments:

Post a Comment