Mashabiki wa Chelsea wamvamia John Terry sababu ni Thibaut Courtois - Darajani 1905

Mashabiki wa Chelsea wamvamia John Terry sababu ni Thibaut Courtois

Share This

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, John Terry ametumia mtandao wa Instagram kumuaga aliyekuwa mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye amejiunga na klabu ya Real Madrid.

Lakini mara baada ya kutuma ujumbe huo ambapo aliandika maneno ya kumsifia na kumuita ni kipa bora duniani kwa upande wake mashabiki wametoa maoni yao kwa kuponda na kutukana alichokiandika gwiji huyo.

Mashabiki wengi wa Chelsea wamekasirishwa kwa kitendo cha kipa huyo raia wa Ubelgiji kulazimisha kuondoka huku akigoma kurejea klabuni kwa tarehe aliyopangiwa na hivyo kuwafanya mashabiki wengi kumuita 'msaliti'

Matusi na kashfa hizo zilizotolewa kwenye ujumbe huo umemfanya gwiji huyo kuzima taarifa kuhusu maoni (turn off comment notifications) kwa ujumbe huo

No comments:

Post a Comment