Msikie Thibaut Courtois alichokisema mara baada ya kujiunga na Real Madrid - Darajani 1905

Msikie Thibaut Courtois alichokisema mara baada ya kujiunga na Real Madrid

Share This

Mlinda mlango raia wa Ubelgiji, Thibaut Courtois amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania uku usajili wake ukiwa na thamani ya paundi milioni 35.

Mlinda mlango huyo ambaye alisajiliwa na Chelsea toka akiwa na miaka 19 aligomea kurejea klabuni Chelsea akishinikiza usajili huu kukamilika.

Mlinda mlango huyo ametumia wasaa wake akiwa anatambulishwa akimuongelea winga wa Chelsea, Eden Hazard ambaye ni mbelgiji mwenzake akisema anatamani siku moja winga huyo ajiunge na Madrid ili acheze nae pamoja tena.

"Hazard amenipongeza kujiunga kwangu na Real Madrid, nami napenda kucheza pamoja naye. Naamini ipo siku atakuja Real Madrid na tutacheza pamoja tena" amesema mlinda mlango huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka sita klabuni huko.

Real Madrid imekuwa ikitajwa kuwafukuzia nyota hao wawili uku ikishindwa kumnasa Hazard kutokana na klabu ya Chelsea kukataa ofa yoyote juu ya nyota huyo.

Courtois alibakiza mkataba wa mwaka mmoja klabuni Chelsea na alishakataa kusaini mkataba mpya uku akikaririwa akisema kama Chelsea ikikataa kumuuza kipindi hiki basi ataondoka bure kwenye dirisha kubwa lijalo kutokana na kufikia muda huo basi mkataba wake klabuni Chelsea ungekuwa ushamalizika.

No comments:

Post a Comment