Hivi unakumbuka ilibaki kidogo nyota wa kibrazil, Robinho kutua Chelsea mwaka 2008? si unakumbuka vizuri kwamba nyota huyo ilibaki kidogo atue Chelsea? unajua kwanini usajili huo ulishindikana na badala yake akajiunga na Man city? basi usijali, ukurasa wa Darajani1905 upo hapa ili kukujuza yote.
Mwaka 2008, nyota huyo raia wa Brazil ambapo jina lake kamili ni Robsob de Souza hakuwa kwenye mahusiano mazuri na klabu yake ya muda huo, Real Madrid na hivyo kuanza kulazimisha kuondoka.
Mchezaji mwenyewe alichagua kuja Chelsea kutokana na ushawishi aliofanyiwa na kocha wa Chelsea kwa kipindi iko, Felipe Scolari ambaye alimhitaji mbrazil mwenzake huyo ajiunge nae ili wafanye makubwa.
"Kiukweli mimi kama mimi nilitamani kutua Chelsea, kwa vile Scolari alinihitaji kuingia kwenye mfumo wake." alisema Robinho.
Hivyo wakati Chelsea inamfukuzia winga huyo, ilimfukuzia ili kutoa nafasi kwa Scolari kutengeneza muhimili mkubwa.
"Nadhani sababu ambayo ilisababisha usajili huu kutokukamilika, ni kwa vile uongozi wa Real Madrid ulikasirishwa kuona jezi za Chelsea zenye jina la Robinho zimeshatengezwa na zimeanza kuuzwa wakati usajili wenyewe haujakamilika." amesema Robinho.
"Lakini pia nadhani kwa vile kwa kipindi kile Chelsea ilikuwa inashiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya hivyo Real Madrid ilikataa kuniuza kwa Chelsea kwa vile inashiriki." amesema Robinho.
No comments:
Post a Comment