Chelsea yamhofia Arrizabalaga kwa Lampard - Darajani 1905

Chelsea yamhofia Arrizabalaga kwa Lampard

Share This
Bodi ya Chelsea yahofia thamani ya Kepa Arrizabalaga kushuka kisa kuwekwa benchi na Frank Lampard.


Hivyo ndivyo tovuti ya Daily Mail ilivyoandika taarifa yake ikieleza kwamba bodi ya klabu hiyo inahofia thamani ya mlinda mlango, Kepa Arrizabalaga kushuka kama kocha Lampard ataendelea kumweka benchi kipa huyo aliyesajiliwa kwa dau lililoweka rekodi ya dunia kama kipa ghali zaidi akisajiliwa kwa paindi milioni 71.


Daily Mail inaamini kwamba kocha Lampard hana mpango wa kuendelea na Arrizabalaga hivyo anataka dirisha kubwa lijalo asajiliwe kipa mwengine.

Kusajiliwa kwa kipa mwengine kutamaanisha Arrizabalaga atafunguliwa mlango wa kuondoka na bodi hiyo ya Chelsea inahofia huenda itamuuza kwa bei ndogo zaidi kama ataendelea kuwekwa benchi.

No comments:

Post a Comment