Habari kuhusu Andre Onana kutaka kujiunga na Chelsea ni habari inatawala na kupamba vichwa vingi vya tovuti na magazeti ya habari za michezo ambapo tovuti maarufu ya Goal.com nayo imeiripoti.
Kupitia mwandishi wake Nizaar Kinsella inaelezwa kwamba mlinda mlango huyo raia wa Cameroon yupo tayari kutua Chelsea na anaamini Chelsea ni mahali sahihi kwake.
Kipa huyo anayekiputa pale klabuni Ajax yupo tayari kukamilisha uhamisho wa kutua Chelsea kama akionyeshwa nia ya kutakiwa na klabu hiyo ya jijini London.
No comments:
Post a Comment