Chelsea yamfata Antonio Conte, yamtaka mshambuliaji wake - Darajani 1905

Chelsea yamfata Antonio Conte, yamtaka mshambuliaji wake

Share This
Kuna taarifa zimeripotiwa na gazeti la Calciomercato la nchini Italia ambalo limeripoti kwamba Chelsea inamfukuzia mshambuliaji nyota, Lautaro Martinez wa klabu ya Inter Milan inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte.

Taarifa hizo zinaihusisha Chelsea kwamba ipo tayari kulipa kiasi cha pesa pamoja na kumtoa mchezaji mmoja ambapo anatajwa ni kati ya Marcos Alonso ama Emerson Palmieri ili kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Argentina.

Nyota huyo mwenye miaka 22 amecheza michezo 20 ya ligi kuu nchini Italia uku akifunga magoli 11 na kutoa pasi ya mwisho 1.

No comments:

Post a Comment