Ligi kuu Uingereza imesimama, ikitoa nafasi kwa wachezaji kupumzika kwenye msimu huu wa baridi. Hii ni mara ya kwanza kwa ligi kuu Uingereza kuwa na ratiba hii.
Hapa nakuletea baadhi ya wachezaji wa Chelsea wakiwa mapumzikoni sehemu mbalimbali.
Marekani;
Willian na familia yake wameenda mapumzikoni nchini Marekani ambapo huko wanafanya matembezi kwa pamoja na kujiweka sawa.
Lakini pia nchini humo yupo Willy Caballero aliyeonekana mara kadhaa akihudhuria michezo ya ligi ya kikapu ya NBA.
Michy Batshuayi pia yupo nchini humo.
Brazil;
Jorginho na familia yake wapo nchini Brazil ambapo huko ndipo alipozaliwa Jorginho licha ya sasa kuitumikia nchi ya Italia.
Umoja wa nchi za Kiarabu (UAE);
Hudson-Odoi, Tammy Abraham, Fikayo Tomori, Reece James, Mason Mount na Ross Barkley, wote kwa pamoja wameonekana kwenye nchi hizo za kiarabu uku Mason Mount akiwa karibu zaidi na Ross Barkley ambapo wameonekana mara kadhaa wakiwa mazoezini kwenye moja kati ya viwanja vinavyopatikana jijini Dubai.
Fikayo Tomori amekuwa karibu zaidi na Tammy Abraham ambaye ameambatana na mpenzi wake, Leah Monroe, wote wakiwa nchini jijini Dubai.
No comments:
Post a Comment