BENITEZ KUUNGANA NA LUIZ - Darajani 1905

BENITEZ KUUNGANA NA LUIZ

Share This

Klabu ya Newcastle united imeingia kwenye vita ya kumuwania mlinzi wa Chelsea, David Luiz anayeonekana kutokuwa na nafasi tena katika kikosi cha Chelsea.

Newcastle iliyochini ya kocha Rafa Benitez aliyewai kuifundisha Chelsea ameingia kwenye vita ya kumuwania nyota huyo raia wa Brazil, ingawa pia usajili huo unaonekana unafanywa ili kumshawishi tajiri mwanamama Amanda Staveley anayetaka kuinunua klabu hiyo ili akamilishe mipango mapema.

Bosi wa Newcastle, Mike Ashley ana mpango wa kuiuza klabu hiyo ambapo mwanamama, Amanda Staveley anataka kuinunua ingawa ana wasiwasi kutokana na mwenendo wa klabu hiyo akihofia inaweza kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment