Kiongozi wa chama cha soka cha nchini Nigeria cha Nigeria Football Federation (NFF), Amaju Pinnick amekijia juu chama cha soka Afrika, CAF mara baada ya kuchaguliwa nyota watatu watakaowania tunzo ya mchezaji bora ambao ni Mohammed Salah raia wa Misri, Pierre Aubameyang wa Gabon na Sadio Mane wa Senegal huku Victor Moses wa Nigeria akitupwa katika orodha hiyo richa ya kuwa na mwaka mzuri akifanya vizuri na timu yake ya taifa na hata akiwa na Chelsea.
Amaju alisema "nimekasirishwa na uteuzi huu, kwanini Moses hayupo? wakati mwaka 2017 amefanya vizuri kuliko hata hao waliochaguliwa"
"Aubameyang amefanya jambo gani kubwa mwaka 2017 na hao wengine?" alihoji kiongozi huyo.
Victor Moses katika mwaka 2017 amefanikiwa kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 huku akiisaidia Chelsea ambayo ndiyo klabu anayochezea kubeba taji la ligi kuu Uingereza na hata kucheza fainali ya kombe la FA la nchini Uingereza.
"sababu iliyomfanya Riyad Mahrez ashinde tunzo hii ya mchezaji bora, kwa vile alifanya vizuri Leicester, kama alivyofanya vizuri Moses. Na kwanini Moses asiwepo" alilalamika Pinnick.
No comments:
Post a Comment