Mlinzi wa zamani wa klabu ya Liverpool, Jamie Carragher ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa michezo katika vyombo vya habari amesema atahudhunishwa kama klabu ya Chelsea itamtimua kocha wake wa sasa, Antonio Conte.
Carragher alisema "naipenda Chelsea iendelee kuwa na Conte, nampenda sana" alisema nyota huyo ambaye ameacha heshima kubwa katika ligi kuu Uingereza na hata kwenye klabu ya Liverpool.
Conte amekuwa akitabiriwa kuwa na msimu mbovu kabla kuanza kwa msimu huku pia baadhi ya vyombo vya habari vikimhusisha na kujiunga na klabu ya Inter Milan ingawa mwenyewe amekuwa akisema bado ataendelea kubaki Chelsea.
No comments:
Post a Comment