Usiku wa leo katika uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea itashuka darajani kumenyana na vijana wa Afc Bournemouth katika kombe la ligi la Carabao Cup katika hatua ya robo fainali, mchezo huo utakaochezwa saa 22:45.
Chelsea itashuka katika mchezo huu ikiwa na historia nzuri dhidi ya klabu hiyo ambapo katika michezo mitano iliyopita imepoteza mchezo mmoja ambapo hiyo ilikuwa mwaka 2015.
Jana katika mkutano wa waandishi wa habari, kocha wa Chelsea, Antonio Conte alisema kuelekea katika mchezo huu atawatumia makinda ambao wanastahili kucheza ambapo kuna uhakika wa Kennedy kuanza katika mchezo huu huku Michy Batshuayi naye akitajwa kuanza katika mchezo huo. Charly Musonda anasumbuliwa na majeruhi hakuna uhakika kama atakuwepo katika mchezo huu.
Endapo Chelsea itashinda mchezo huu basi kuna uwezekano nusu fainali ikakutana na Manchester city au Arsenal waliofuzu jana.
No comments:
Post a Comment