EXCLUSIVE; MORATA KUADHIBIWA - Darajani 1905

EXCLUSIVE; MORATA KUADHIBIWA

Share This

Nyota wa Chelsea, Alvaro Morata ameadhibiwa kutokana na tukio lake la ushangiliaji akiuweka mpira tumboni na kuonyesha ishara ya kutarajia kupata mtoto akimaanisha kufurahishwa na mpenzi wake kupata ujauzito, ambapo kwa tukio hilo lililompatia kadi imeelezwa ataadhibiwa.

Baada ya kufunga goli lililoihakikishia Chelsea kufuzu hatua ya nusu fainali katika dakika ya 90+ nyota Alvaro Morata aliuchukua mpira na kuuweka ndani ya fulana katika sehemu ya tumbo akionyesha kufurahia kwa mke wake, Alice Campelo kupata ujauzito. Ambapo kwa tukio hilo lilimfanya kupewa kadi ya njano na kumfanya kutimiza kadi 5 za njano zinazomaanisha kuukosa mchezo unaofata wa ligi kuu dhidi ya Everton.

Ambapo ishahakikishwa kwa tukio hilo Alvaro Morata ataukosa mchezo wa ligi kuu utakaochezwa jumamosi dhidi ya Everton.

No comments:

Post a Comment