Goli la dakika za majeruhi lililofungwa dakika ya 90, likifungwa na Alvaro Morata ndilo linaivukisha Chelsea katika hatua ya robo fainali ikiifunga Afc Bournemouth magoli 2-1.
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Willian Borges akipokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo mhispania fundi wa pasi, Cesc Fabregas, shambulizi likitengenezwa vizuri na beki mbrazili, Kennedy na Willian kuifungia Chelsea goli la kwanza, hiyo ikiwa dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza. Na mpaka mpira unaenda mapumziko, Chelsea ilikuwa mbele kwa mabao 1-0.
Kipindi cha pili kulifanyika mabadiliko kadhaa huku Hazard na Bakayoko wakiingia kuchukua nafasi za Willian na Pedro na Morata pia kuingia baadae.
Mara baada ya muda kwenda zaidi, Afc Bournemouth walichomoa goli, likifungwa na Gosling akipokea pasi ya Ibe na kufanya mchezo kuwa 1-1, kabla ya Chelsea kufanya shambulizi la kushtukiza katika dakika hiyohiyo ya 90, na ubora wa Alvaro Morata na Eden Hazard ukionekana kuwa mzuri ambapo Eden Hazard alitoa pasi ya kisigino kumpasia Morata na mhispania uyo kufunga goli la pili na la nyongeza na kuifanya Chelsea kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo majirani zetu, Manchester united wameshindwa kufuzu mara baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Bristol City, cha mabao 2-1.
Sasa Chelsea itakutana na mmoja kati ya hawa Arsenal, Manchester city au Bristol city katika hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment