HAZARD KUTIMKIA MADRID - Darajani 1905

HAZARD KUTIMKIA MADRID

Share This

Kuna habari katika mitandao zimesambaa zikieleza nyota wa Chelsea, Eden Hazard anakaribia kuachana na Chelsea na kujiunga na mabingwa wa dunia, Real Madrid.

Habari zinadai Eden Hazard amefikia katika mazungumzo ya mwisho na mabingwa hao ambapo kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane anatajwa kumfanya Hazard kuwa chaguo lake la kwanza akimtaka kwa nguvu zote atue klabuni hapo.

Lakini kinda na nyota wa Real Madrid, Marco Asensio amesema kama Hazard akisajiliwa klabuni hapo basi yeye ataachana na klabu hiyo na kuondoka.

Hazard alisajiliwa na Chelsea mwaka 2013 akitokea Lille ya Ufaransa na kufanikiwa kushinda mataji na tunzo binafsi nyingi akiwa Chelsea.

No comments:

Post a Comment