Mara baada ya jana kukamilisha usajili wake wa kuungana na Chelsea, nyota mpya wa klabu hiyo, Emerson Palmieri amefanya mahojiano akihojiwa kwa mara ya kwanza toka asaini mkataba huo mpya utakaomweka klabuni kwa miaka minne na nusu huku akilipwa fungu la paundi 45,000 kwa wiki.
"Toni (Antonio Rudiger) na mimi tumecheza wote tukiwa Roma kwa miaka miwili. Kikubwa nachoweza kukisema kuhusu yeye ni mtu makini na bora sana, na hilo ameshalionyesha akiwa hapa Chelsea, kwa hiyo nitajihisi kuwa na furaha kurudi kucheza sambamba pamoja naye" alijibu hivyo alipoulizwa juu ya mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger ambaye alicheza na mlinzi huyo wa kushoto pindi walipokuwa wote klabuni As Roma.
"Chelsea dhidi ya Barcelona mara zote huwa ni mchezo mgumu na nakumbuka niliangalia mchezo huo kipindi kile wakati Chelsea ilipotwaa klabu bingwa, na ilimtoa Barcelona. Kila mtu alishuhudia mchezo huo na ubora wake na naamini kwa mara hii itakuwa ni mara mbili zaidi ya ile. Naamini tutashinda" alijibu alipoulizwa juu ya maoni yake katika mchezo wa hatua ya 16-bora ambapo Chelsea itapambana na Barcelona.
"Kiukweli najiona naenda kuwa bora zaidi nikiwa hapa, nikiwa chini ya Antonio Conte. Yeye ni mtu mmoja ambaye tayari ashadhihirisha kuwa ni bora na kila mtu anayecheza chini yake huwa anakuwa ni mchezaji bora kwa hiyo nami nimefika hapa ili kulitimiza hilo, kwa hiyo naamini naenda kuwa chini ya moja ya makocha bora duniani" alisema nyota huyo alipoulizwa nafikiri atakuwaje akicheza chini ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte.
"Kiuhalisia najihisi nimepona kabisa. Majeruhi niliyoyapata sasa ni historia, ilikuwa kipindi kigumu sana kwangu kwa kuwa nilikuwa majeruhi kwa miezi sita lakini jambo la muhimu zaidi ni sasa kuwa mzima na afya njema. Lakini ili kujihisi vyema kabisa ni pale nitakapoungana na wenzangu ili kuanza mazoezi na kuisadia klabu yangu" alimaliza nyota huyo akijibu mara kuhusu majeruhi aliyoyapata yaliyomweka nje kwa miezi sita.
No comments:
Post a Comment