Habari muhimu;
Chelsea; Chelsea itashuka uwanjani leo lakini ikiendelea kumkosa mshambuliaji wake, Alvaro Morata aliyepata majeraha lakini pia kuna taarifa zinasema mshambuliaji mbadala, Michy Batshuayi asubuhi ya leo amesafiri kwenda nchini Ujerumani ili kukamilisha usajili wake wa mkopo katika klabu ya Borrusia Dortmund, kwa maana hiyo huenda Chelsea leo ikatumia mfumo wa 3-5-2 ambapo kwa nafasi au safu ya ushambuliaji anaweza akatumika Eden Hazard pamoja na Pedro Rodriguez huku Willian naye akiwa mmoja wa wachezaji watakaoukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi pamoja na mbrazili mwenzake, David Luiz ambaye naye alipata majeruhi siku mbili kabla ya mchezo uliopita dhidi ya Newcastle united.
Lakini habari njema ni Cesc Fabregas na mlinda mlango namba moja, Thibaut Courtois wote kuwa sawa na kupona kabisa na kuna uwezekano wakatumika kwenye mchezo wa leo huku nyota mpya Emerson Palmieri anaweza akatambulishwa kwa mashabiki usiku wa leo mara baada ya kusajiliwa rasmi na Chelsea usiku wa jana.
Bournemouth; Hawa majamaa leo watashuka Darajani huku wakiwakosa nyota wao kadhaa ambao ni pamoja Jermaine Defoe pamoja na Thyrone Mings kutokana na majeraha lakini nyota wao wengine kama Joshua Kings na Junior Stanslaus watakuwepo uwanjani.
Mwamuzi; Lee Probert ndiye atakuwa mwamuzi wa kati kati mchezo wa leo ambapo huu ndio utakuwa mchezo wa kwanza kwa mwamuzi huyo kuamua dhidi ya Chelsea ambapo mpaka sasa ameshachezesha na kuamua kwenye michezo 20 na ametoa kadi za njano mara 30 na kadi nyekundu 4.
Rekodi; Licha ya kuwa na uhusiano mzuri kwenye kuuziana wachezaji haswa mpaka sasa Burnemouth imeshahusishwa na nyota wengi kutoka Chelsea, na kama una kumbukumbu vizuri iliwai kumtaka mpaka John Terry mara baada ya nyota huyo kuachana na Chelsea na kuwa kwenye mipango ya kutafuta timu nyengine msimu uliopita, ila Chelsea haijataka mahusiano mzuri haswa linapokuja swala la matokeo. Katika michezo 11 ambayo Chelsea imecheza dhidi ya klabu hii imeibamiza mara 9 na kupoteza mara mbili.
Mechi zilizopita;
Chelsea: DDWLW
Bournemouth; DDWWD
Muda; Saa 10:45 usiku (Saa 22:45) kwa saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment