Chelsea leo itashuka uwanjani Stamford Bridge kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Norwich city kwenye kombe la FA mara baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Carrow road kuisha kwa suluhu ya 0-0.
Kama timu yoyote ikifanikiwa kushinda mchezo wa leo itapambana dhidi ya Newcastle katika mchezo ujao wa hatua ifuatayo.
Habari muhimu;
Chelsea; Cesc Fabregas ataukosa mchezo huu mara baada ya kupata majeruhi, naye Gary Cahill akiwa na maumivu ya ndani kwa ndani naye ataukosa mchezo huu huku kwa Ross Barkley aliyetegemewa kucheza mchezo huu ukiwa ndio mchezo wake wa kwanza toka asajiliwe klabuni Chelsea hatoruhusiwa kucheza mchezo huu kutokana nasheria inavyosema ikionekana alichelewa kukamilisha usajili, na hivyo haruhusiwi.
Lakini pia majukumu ya kuvunja rekodi mbaya ya kutokupata goli katika michezo mitatu leo atakabidhiwa Michy Batshuayi ambaye yeye ndiye atatumika kama mshambuliaji wa mwisho kucheza kama mshambuliaji namba 9.
Lakini pia kuna uwezekano mkubwa kwa Ethan Ampadu kuanza katika mchezo wa leo ambaye atakuwa kwenye mpango wa kufanya mabadilishano kwa wachezaji ili wengine wapate kupumzika kutokana na mfululizo wa mechi nyingi kwa muda mfupi.
Norwich; Tangu ilipopata suluhu dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa kwanza wa kombe hili la FA, wamekuwa na mwendelezo mzuri wakitoka kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Bristol city ambapo Norwich ilikuwa ugenini ambapo kwa matokeo hayo imekuwa hawajafungwa au kupoteza mchezo wowote kwa michezo mitano iliyopita huku wakiruhusu kufungwa goli moja tu. Kwa rekodi hiyo wanaweza kufika Stamford Bridge kwa kujiamini.
Mwamuzi; Graham Scott, kwa sasa ana miaka 49 akiwa mmoja wa waamuzi wenye umri mkubwa.
Rekodi;
Chelsea; WDDDD
Norwich; WDWDW
Muda; Saa 10:45 Usiku(Saa 22:45)
No comments:
Post a Comment