Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekataa kuzungumzua tetesi za klabu yake kumnyatia nyota raia wa Chile, Alexis Sanchez ambaye anatajwa kufukuziwa na klabu kadhaa vigogo pale Uingereza huku Chelsea ikitajwa nayo kumuwania.
Sanchez mwenye miaka 29 kwa sasa kiwa amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake wa sasa wa kuitumikia klabu anayoichezea ya Arsenyani(Arsenal) anatazamiwa kuondoka klabuni hapo.
"Siwezi kuongelea vitu ambavyo najua haviwezi kutokea, yanini nipoteze maneno yangu kumuongelea mtu ambaye najua hawezi kusajiliwa" alisema kocha Antonio Conte ilipoulizwa juu ya Chelsea kumuwania winga huyo..
**Kutokana na kauli hii, naona kama ina utata, je Conte anasema hawezi kuongelea usajili wa nyota ambao hadhani kama watasajiliwa au anajua kuwa bodi haiwezi kuukamilisha usajili huu maana alishawai kukiri kuwa Sanchez ni mmoja wa nyota anaowapenda?
Conte hana majukumu ya kufanya usajili klabuni Chelsea, na badala yake yeye hutoa taarifa tu kwamba anamuhitaji mchezaji flani na flani, lakini bodi ya Chelsea ikiongozwa na mwanamama Marina Glanovskaia wao ndio wanahusika na usajili.
Lakini pia huenda anadhani uwezekano wa nyota huyo kutua Chelsea ni ngumu kutokana na mahitaji ya usajili wake na hata mahitaji binafsi ya nyota huyo!
Una majibu gani katika hili?
No comments:
Post a Comment