HUDSON-ODOI NI NANI? - Darajani 1905

HUDSON-ODOI NI NANI?

Share This
Huenda jana ulishangazwa na kiwango alichokionyesha kijana wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi aliyeingia kuchukua nafasi ya Pedro katika dakika ya 81. Ulikuwa ndio mchezo wa kwanza kwa kinda huyo kuichezea Chelsea ya wakubwa.

Lakini je unajua katokea wapi? Je unataka kufahamu chochote kuhusu Odoi? Hapa nakujuza kwa udogo mambo ambayo unayopaswa kuyajua juu ya nyota huyu.
Jina lake kamili anaitwa Callum James Hudson-Odoi ambaye kwa sasa ana miaka 17 na akiwa na asili ya Ghana pia ndio maana unaona hata hilo jina la Odoi lina kama Uafrika ndani yake, na kama haujajua ni mdogo kuliko nyota mwengine wa Chelsea, Ethan Ampadu ambapo Odoi alizaliwa mwezi Novemba mwaka 2000 wakati kwa Ampadu alizaliwa mwezi Septemba mwaka huohuo 2000. Kwa hiyo Ampadu amemzidi huyu miezi miwili.

Hudson-Odoi ni mshambuliaji na haswa anacheza kama mshambuliaji wa kati, na jambo la kuvutia ambalo labda hulijui, nyota huyu anaichezea Chelsea ya vijana chini ya miaka 23 huku mwenyewe akiwa na miaka 17, kutokana na uwezo wake mkubwa haimpi tabu kucheza na wachezaji waliomuacha umri mpaka kwa miaka mitano.

Alitua Chelsea mwaka 2007 kipindi iko alikuwa akicheza kwenye timu ya watoto chini ya miaka 8 licha ya udogo wake kiumri ila alikuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu na kuzifanya vile apendavyo na huku akitengeneza magoli mengi pia. Alikuwa akisifiwa kutokana na kipaji chake na uwezo wake mkubwa huku akiwa na sifa ya kucheza nafasi yoyote anayopangwa kwenye ushambuliaji.

Akiwa na nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha vijana wa Chelsea huku akiisaidia kutwaa mataji kadhaa huku mwenyewe akihusika vyema kwenye ufungaji magoli huku akisaidia pia katika utengenezaji nyota na mpaka kufikia hatua kuchaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 17 kilichoshiriki michuano ya Ulaya ambapo kwa bahati mbaya Uingereza ilipoteza kwa matuta mbele ya timu ya Hispania.

Lakini alichaguliwa tena kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2017 chini ya miaka 17 ambalo kama unakumbuka vyema vijana wetu wa Tanzania (Serengeti Boys) walibakiza hatua kidogo kuweza kucheza michuano hii iliyofanyika nchini India na timu ya taifa ya Uingereza ilifanikiwa kuwa mabingwa huku Hudson-Odoi akicheza michezo yote katika michuano hiyo huku katika mchezo wa fainali wakiibamiza Hispania 5-2 ili kulipiza kisasi. Na kufanikiwa kuwa mabingwa wa Dunia kwa mwaka 2017.

Nyota huyo jana aliichezea Chelsea ya wakubwa mchezo wake wa kwanza huku akionyesha kiwango bora, na sisi kama mashabiki wa Chelsea tunategemea kuyaona makubwa kutoka kwake.

No comments:

Post a Comment