MKONGWE AMWAMBIA MAHREZ ATUE CHELSEA - Darajani 1905

MKONGWE AMWAMBIA MAHREZ ATUE CHELSEA

Share This
Nyota wa klabu ya Leiceser city iliyochini ya mmiliki wkutoka barani Asia, Riyad ahrez anatajwa kuwaniwa na baadhi ya klabu katika dirisha la usajili la mwezi huu Januari huku Chelsea nayo ikitajwa kumfukuzia nyota huyo raia wa Algeria.

Nyota huyo alikuwepo kwenye mchezo wa jumatano iliyopita mara baada ya Chelsea kushuka uwajani kumenyana na Arsenyani (Arsenal) ambapo kwa uwepo wak ilidaiwa huenda alikuwa akijiandaa kutua klabu moja wapo kati ya hizo kutokana pia na kuhusishwa na klabu hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Arsenyani , Ray Parlour ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka alihojiwa juu ya nini anakiona juu ya mchezaji huyo aliyekuwa mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2015-2016 huku akiiongoza klabu yake kutwaa taji la ligi kuu nchini humo "Kwanza nashangazwa na kuendelea kubaki klabuni pale. Kwa kuwa ni mchezaji nyota. Kuna kipindi alikuwa hachezi vizuri ila kwa sasa amerudia ubora wake. Huyu ndiye aliyeipatia Leicester taji la ligi kuu akishirikiana vyema na Jamie Vardy"

"Ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi tofauti. Najua kama klabu yangu ya zamani imekuwa ikitajwa kumuwania, na huko ndiko anapotakiwa kuangalia kwa sasa, anatakiwa aangalie klabu gani itamfaa katika zile klabu sita za juu. Anaweza akang'aa ata akiwa Chelsea" alisema mkongwe huyo.

faida mojawapo ambayo Chelsea inaweza kuitumia kumnasa nyota huyu ni kwamba klabuni Chelsea kuna nyota wawili ambao walicheza na Mahrez pindi walipokuwa Leicester ambao ni Danny Drinkwater pamoja na N'golo Kante kama ikiwa tayari kumnasa nyota huyo basi inaweza kuwatumia hao ili wafanye ushawishi kwa Mahrez lakini pia faida kwa timu itakayompata nyota huyu kwa dirisha hili la usajili, itaweza kumtumia kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya kutokana na nyota huyo kutoshiriki msimu huu, tofauti na kama Chelsea ikimnasa Edin Dzeko ambaye yeye hatoruhusiwa kuichezea Chelsea katika michuano hiyo kama ikifanikiwa kumnasa.

No comments:

Post a Comment