MAMBO 8 MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs LEICESTER - Darajani 1905

MAMBO 8 MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs LEICESTER

Share This
Chelsea inashuka uwanjani jioni ya leo ya raundi ya 23 ya ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea itauwa nyumbani kupambana na klabu ya Leicester city ambayo inashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku Chelsea ikishhika nafasi ya tatu ikiwa na alama 49.

Hapa nimekuletea mambo 8 unayopaswa kuyajua 
 1. Leicester city wamepoteza michezo 12 kati ya 14 dhidi ya Chelsea katika mashindano yote huku akipata ushindi mara moja tu msimu wa 2015/2016 iliposhinda nyumbani na kutoa sare ugenini.
2. Chelsea imepoteza mara moja tu kati ya michezo 26 ilipocheza dhidi ya Leicester kwenye uwanja wa Stamford Bridge tangu mwaka 1965. Ambapo Leicester walishinda 2-0 mwaka 2000. Chelsea imeshinda michezo 16 ikitoa suluhu michezo 9 na kfungwa mchezo mmoja.
3. Antonio Conte ameshinda michezo 25 kati ya michezo yake 30 katika ligi kuu Uingereza tangu amefika Chelsea, ameungana na waliomtangulia klabuni hapo ambao ni Jose Mourinho, Carlo Ancelotti ambao kwa pamoja walishindwa kushinda mchezo wa 31 uwanjani hapo.
4. Chelsea haijapoteza mchezo wowte katika michezo 6 iliyopita katika ligi kuu Uingereza iwe nyumbani au ugenini, ikivuna alama 14 kati ya 18.
5. Marcos Alonso wa Chelsea amefunga magoli 12 toka msimu uliopita, ndio magoli mengi kufungwa na mlinzi mpaka sasa kwa misimu hiyo miwili
6. Leicester city hawajapata ushindi wowte katika michezo 12 ya ligi kuu ilipocheza ugenini dhidi ya timu sita za juu.
7. Jamie Vardy amezifunga timu 6 za juu magoli 22 kati ya michezo 41 kwenye ligi kuu toka alipocheza mchezo wa kwanza kwenye ligi hiyo mwaka 2014.
8. N'Golo Kante na Danny Drinkwater wote walizichezea Leicester city kwa pamoja huku kila mmoja akiichezea klabu hiyo zaidi ya michezo 35 msimu ambao walikuwa mabingwa wa ligi kuu, 2015/2016. 

No comments:

Post a Comment