PL; FT, CHELSEA 0-0 LEICESTER - Darajani 1905

PL; FT, CHELSEA 0-0 LEICESTER

Share This

Ni sare nyengine inapatikana kwa Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge, ikiwa ni sare ya pili  kwa mashindano yote kupatikana katika uwanja huo tangu ilipopata ushindi wake wa mwisho dhidi ya Brighton, lakini pia inakuwa sare ya nne kuipata Chelsea mfululizo toka ilipopata ushindi katika mchezo huo lakini pia inakuwa ni sare ya tatu mfululizo kuipata Chelsea bila kufunga goli lolote.

Inaonekana kuna tatizo katika safu ya ushambuliaji ambapo katika mchezo huu imeshindwa kutengeneza nafasi za mabao ambapo katika mchezo wa leo ambao Leicester walicheza wakiwa pungufu kwa dakika 22 kutokana na mchezaji wao kupewa kadi nyekundu Chelsea imeishia kupiga mashuti 5 tu huku machache yakiwa yameelekea golini.

Chelsea haikuwa na kiwango kizuri, ilicheza ovyo tangu kipindi cha kwanza ambapo katika kipindi hicho Leicester walimiliki mpira kwa asilimia ya chini huku Leicester wakilikamia lango la Chelsea kwa asilimia kubwa.

Huenda tatizo lipo kwenye mfumo anaoutumia kocha, mfumo wa 3-5-2 unaonekana kutoendana na Chelsea kabisa ambapo Chelsea ilianza kuutumia mfumo huo tangu mpira unaanza, na ilianza kumiliki mpira pale tu ulipoanza kutumika mfumo uliozoeleka wa 3-4-3 mara baada ya Willian na Pedro kuingia kuchukua nafasi za Fabregas na Hazard.

Nadhani katika hili kocha inabidi alifanyie ufumbuzi kwa kutumia mfumo ule uliozoeleka ambao uliisaidia Chelsea ikabeba taji la ligi kuu msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment