MORATA NA DZEKO, NANI KUWA CHAGUO LA KWANZA CHELSEA? - Darajani 1905

MORATA NA DZEKO, NANI KUWA CHAGUO LA KWANZA CHELSEA?

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kwa karibu kumvuta nyota wa klabu ya As roma, Edin Dzeko ambaye amekuwa akitajwa kusajiliwa kwa kiasi cha Euro milioni 50 pamoja na nyota mwenzake klabuni hapo, Emerson Palmieri ambaye yeye ni mlinzi wa kushoto.

Kutokana na kuhusishwa na nyota huyo, mchambuzi wa michezo wa Sky Sports, Paul Merson ametoa neno juu ya uwepo wa nyota huyo raia wa Bosnia, itakuwaje kama akitua klabuni? Je kati yake na mshambuliaji wa sasa wa Chelsea, Alvaro Morata nani atatumika kama chaguo la kwanza?

"Ninadhani chaguo kubwa la Chelsea katika dirisha hili la usajili ni mshambuliaji wa kati. Michy Batshuayi alicheza vizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Brighton, lakini sidhani kama atakuwa ni jibu sahihi kama Alvaro Morata akipata majeraha makubwa."

"Kama Edin Dzeko akitua nadhani atatumika kama mshambuliaji wa kikosi cha kwanza na sio kuwa mbadala wa Morata., ambapo hiyo itafungua milango kwa Batshuayi kuondoka"

"Je wanaweza kumpata nyota mwengine atakayeweza kuongeza nguvu kwenye kikosi? Sina uhakika. Kwa timu kubwa kama Chelsea inapomsajili mtu inategemea kumpata mtu atakayekuwa kwenye uwezo wa juu wa kucheza kwenye mechi hata 10 mfululizo lakini sioni mchezaji wa aina hiyo kupatikana katika dirisha hili la mwezi januari"

"Watalazimika kukiimarisha kikosi chao zaidi katika dirisha kubwa linalokuja, nategemea wataweza hata kupambana kuziba au kupunguza pengo la alama kati yake na Man city" alisema mchambuzi huyo.

Je unakubaliana nae?


No comments:

Post a Comment