100K, ASANTENI SANA - Darajani 1905
Jambo la kwanza na la muhimu kabisa ni kusema asante kwa Muumba wa Mbingu na nchi, kwa kunifikisha mpaka siku ya leo na kuniwezesha kufikia hatua hii ambayo kwangu naona ni mafanikio ya hali ya juu. Ukurasa au blog ya Darajani 1905 imefikisha watazamaji wa jumla laki moja (100,000) ambapo ni hatua kubwa maana ni muda wa mwezi mmoja na siku 18 tuzimeuchukua ukurasa huu kufikia mafanikio haya.

Muhimu ni kusema asanteni kwa kila aliyeshiriki katika mafanikio haya maana bila nyinyi hamna kitu, asanteni sana mashabiki wa Chelsea duniani kote ambapo kwa nchi tano zinazoongoza kutazama ukurasa huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Marekani, Indonesia pamoja na India.

Napenda kufurahia siku hii ya muhimu kwangu na hata kwa blog hii ambayo bila nyinyi isingefikia hapa ilipo, asanteni sana pia kwa mashabiki wa timu pinzani maana hata nyinyi pia mmekuwa wa muhimu katika ukurasa huu kufikia hapa ulipofikia. Kama navyosemaga kila siku, raha ya majirani ni kutaniana na kufurahi pamoja, najua niimekuwa nikitumia majina ya kiutani kuripoti habari zenu lakini ndio utani ulivyo na ndivyo tunavyozidi kurifurahia soka kwa namna nyengine tofauti na kulicheza uwanjani. Nasema pia asanteni kwenu na tupo pamoja.

Mpira sio vita, mpira unatuleta pamoja na kutufanya tuwe kitu kimoja kama alivyoimba marehemu Lucky Dube akisema 'One people, different colors' akimaanisha Tofauti yetu ni rangi tu, ila sisi wote ni binadamu


No comments:

Post a Comment