Klabu ya Chelsea imehusishwa kwa karibu na kocha wa zamani wa timu ya Barcelona, Luis Enrique ambaye kwa sasa hana timu na Chelsea imetajwa katika mpango wa kumsajili kocha huyo.
Kutokana na kuhusishwa kwake na kumtaka kocha huyo, inaelezwa kuwa mazungumzo baina ya pande mbili kati ya upande wa Chelsea na upande wa kocha huyo kuwa yamefikia pazuri na ilikuwa ikitazamiwa kocha huyo kujiunga na Chelsea muda wowote kabla ya kutoka taarifa kuwa kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte kuwa amepewa muda zaidi.
Lakini kutua kwa Luis Enrique klabuni Chelsea basi kutatanguliwa au inabidi ifanyike iwezekanavyo ili Chelsea imsajili mshambuliaji wa klabu ya Barcelona ambaye kocha huyo aliwai kumfundisha klabuni hapo, Luis Suarez.
Kocha Enrique anamtaka nyota huyo raia wa Uruguay ili ajiunge na Chelsea kabla au baada ya kuwa kocha rasmi wa Chelsea wakati huohuo kumetoka taarifa zinazosema chanzo cha kocha huyo kukataa kuinoa Chelsea katika kipindi hiki cha katikati ya msimu ni kutokana na benchi lake la ufundi kuwa kwenye majukumu katika klabu nyengine na hivyo inakuwa ngumu kuungana nae kocha huyo mpaka mwisho wa msimu.
No comments:
Post a Comment