Kocha Antonio Conte leo amefanya mkutano na waandishi wa habari ambapo huwa anafanya hiyo kila Chelsea inapokuwa inaelekea kucheza mchezo wake ambapo jumatu itacheza dhidi ya West Bromwich Albion ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kucheza mchezo huo wa ligi kuu Uingereza.
hapa nakuletea baadhi a aliyoyasema kwenye mkutano huo alioufanya jioni ya leo katika uwanja wa mazoezi wa Cobham Stadium
Alipoulizwa juu ya kuwaruhusu wachezaji kupumzika kwa siku mbili mara baada ya mchezo uliopita dhidi ya Watford, koch aAntonio Conte alisema "nadhani ndi kipindi pekee walichokipata ili kupumzika kwa msimu huu, michezo imekuwa mingi na kuwafanya wakose kabisa muda wa kupumzika na kuwa sawa. Nadhani mnatambua tunashiriki michuano mingi msimu huu, ni tofauti na msimu uliopita, nadhani ingekuwa sahihi kama chama cha soka cha Uingereza (FA) kingefanya utaratibu mzuri katika kupanga ratiba, sio kwa wachezaji wangu tu wanaokosa muda wa kupumzika ila wachezaji wote kwa ujumla"
Alipoulizwa juu ya kauli aliyoitoa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Watford ambapo mara baada ya mchezo alisema kuwa wachezaji wamecheza chini ya kiwango lakini pia wamecheza wakiwa na uoga, alisema "Ukiangalia kwa michezo hu miwili iliyopia, hatukucheza sawa kabisa katika mchezo dhidi ya Watford. Ni tofauti na Bournemouth maana tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini katika mchezo dhidi ya Watford hatukucheza soka safi na hatukutengeneza nafasi, hatukuwa na hali nzuri kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wa mchezo"
Alipoulizwa juu ya kiwango cha Tiemoue Bakayoko ambaye anaonekana kushindwa kuendana na soka la Uingereza, kocha Antonio Conte alisema "Bado ni kijana mdogo, na ana umri mdogo, lakini usisahau msimu uliopita alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu nchini Ufaransa akiwa na Monaco, lakini pia walifanikiwa kufika mbali katika klabu bingwa. Ni ngumu kuzoea mapema soka la ugenini haswa kwa Uingereza, muhimu kwake najariobu kumsaidia na kumweka sawa, lakini sio kumsaidia yeye tu, ila kwa kila mchezaji"
Alipoulizwa juu ya majeruhi, alisema "Hakuna majeruhi wapya, lakini kama unavyojua wengi walikuwa kwenye mapumziko, na leo ndio tumeanza mazoezi kwa maana hiyo wengi wapo kikosini kujiandaa dhidi ya West Brom"
Alipoulizwa juu ya majeruhi ya Pedro, Morata na Christensen, alisema "Hapana, Pedro sio majeruhi na yupo sawa kwa ajili ya mchezo huo, lakini ukiniuliza juu ya Morata nakosa cha kujibu maana bado sijajua lini atarejea uwanjani, iwe kwa mwezi mmoja au hata msimu mzima, bado sijajua lakini tunajitahidi kumfanya apone haraka majeruhi yake ya mgongo, kuhusu Christensen anaendelea vizuri na tayari ameanza mazoezi lakini bado hajawa sawa kabisa"
Alipoulizwa juu ya Chelsea kumhitaji Michy Batshuayi ambaye kwa sasa yupo Borrusia Dortmund kwa mkopo alisema "Dirisha la usajili lishafungwa na hakuna haja ya kuongelea kuhusu hilo, muhimu ni kuwatumia wachezaji waliopo ili kuleta mafanikio"
Alipoulizwa juu ya kubadili mfumo ambao unatumika na Chelsea kwa sasa, yaani mfumo wa 3-4-3 na kutumia wa 3-5-2 alisema "hata kwenye mchezo dhidi ya Watford tulitumia mfumo huo, lakini bado tukaruhusu magoli matatu ndani ya dakika nane kwa hivyo sijaona tatizo kwenye mfumo"
Hayo ni baadhi ya aliyoyaongea hivi leo kuelekea mchezo huo wa raundi ya 27 ya ligi kuu Uingereza.
ALICHOKISEMA KOCHA ANTONIO CONTE KUELEKEA CHELSEA vs WBA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment