Mara baada ya mshambulaji wa Chelsea kipindi iko, Fernando Torres ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya nchini Hispania, Atletico Madrid, alikuwa hayupo kwenye ubora wake akisajiliwa kutokea klabu ya Liverpumba (Liverpool) ambako huko alikuwa na uwiano mzuri wa kufunga magoli mpaka kubatizwa jina la El Nino, ikimaanisha zile mvua kali kutokana na kufunga kwake magoli.
Torres alikuwa akicheza mchezo huu huku akihesabiwa kati ya wachezaji walioshuka kiwango, lakini kioja kilitokea pale mlinzi wa Chelsea, David Luiz alipomfata nyota huyo na kumuombea wakati wakiwa uwanjani, cha ajabu mara baada ya maombi, Torres akafunga magoli mawili katika mchezo huo ulioisha kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao 4-2 ikiwa nyumbani Stamford Bridge mwaka 2011.
Maombi yalifanya kazi.😂😂😂
No comments:
Post a Comment