Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye ni raia wa Hispania anatajwa kutokuwa na furaha dhidi ya benchi la ufundi la timu yake ya taifa mara baada ya jina lake kutochaguliwa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza michezo ya kirafiki ya kimataifa katika mwezi huu, michezo iliyoko kwenye kalenda ya FIFA.
Kutokuwa na furaha kwa nyota huyo kumefichuliwa na mchezaji mwenzake klabuni Chelsea, Marcos Alonso ambaye ni muhispania mwenzake ambaye yeye amechaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia kwenye kikosi hicho ambapo alipohojiwa juu ya nyota mwenzake huyo alisema kuwa nyota huyo hana furaha kwa sasa mara baada ya jina lake kuachwa kwenye kikosi hicho lakini anaamini atarudia kwenye ubora wake aliokuwa nao mwanzo mara baada ya kutokuwa sawa kimchezo kwa muda sasa.
Alvaro Morata aliifungia Chelsea goli lake la kwanza siku ya jumapili katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Leicester, ambapo limekuwa goli lake la kwanza toka alipofunga goli la mwisho tarehe 26-Desemba mwaka jana licha ya kuanza msimu kwa moto akifunga magoli nane katika michezo nane ya kwanza.
No comments:
Post a Comment