VIJANA WA CHELSEA WAUNGANA TENA - Darajani 1905

VIJANA WA CHELSEA WAUNGANA TENA

Share This
Kama umekuwa mfuatiliaji wa mtandao wa Instagram kuna video ya tukio ilitumwa na nyota wa Chelsea. Ola Aina ambaye anaichezea klabu ya Hull city kwa mkopo ambapo video hiyo ilikuwa ikimuonyesha nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi wa kulia akiwa na nyota wenzake wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek ambaye anaichezea klabu ya Crystal Palace kwa mkopo, Nathaniel Chalobah ambaye alikuwa mchezaji wa Chelsea ingawa kwa sasa ameuzwa na kwenda klabu ya Watford, Nathan Ake ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Afc Bournemouth ambaye alishawai kupita Chelsea wakiwa katika mgahawa fulani wakipata chakula cha usiku.

Huu ni muunganiko wa nyota hao ambao wameamua kuungana na kupata pamoja chakula cha usiku huku wakifurahia kuzaliwa kwao na kukulia kwao kwenye klabu moja ya nchini Uingereza inayopatikana magharibi mwa jiji la London kwenye mitaa ya Fulham, Chelsea FC.

Hongereni vijana, ado tunaaminimtarudi Chelsea na kuijenga ili kuwa imara zaidi...

No comments:

Post a Comment