Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia kiungo raia wa Ivory Coast, Jean Michael Serri ambaye anaichezea klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) klabu ya OGC Nice licha ya nyota huyo kuzivutia klabu nyengine barani Ulaya
Gazeti moja barani Ulaya limetoa ripoti likisema Chelsea ndiyo klabu inayoongoza kuwania saini ya nyota huyo huku ikipata upinzani kutoka kwa klabu kama Arsenal ambayo imeshindwa kufikia makubaliano katika usajili huo pamoja na klabu inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho, klabu ya Manchester united.
Licha ya Chelsea kuwa na kizungumkuti kwenye kumsaka kocha mpya atakayeweza kumrithi kocha wa sasa, Antonio Conte lakini bado gazeti hilo linaitaja Chelsea kuwa klabu inayoongoza katika mpambano wa kumnasa kiungo huyo mwenye miaka 26.
No comments:
Post a Comment