Alitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 akitokea nchini kwao Hispania ambapo huko alikuwa akiichezea klabu ya Real Madrid na mpaka sasa wakati msimu ukiwa umeisha amefanikiwa kuifungia Chelsea magoli 15 tu katika michuano yote akihusika vyema kwenye safu ya ushambuliaji ingawa amekuwa akipata malalamiko mengi kwa kushindwa kutimiza majukumu na kuonyesha uwezo mkubwa haswa kwenye umaliziaji wa mashambuliaji.
Alvaro Morata anatajwa na gazeti la nchini Italia, Gianluca di Marzio kwamba anajuta kufanya uamuzi wa kutua Chelsea katika usajili wa dirisha kubwa lililopita wakati alipokuwa akitakiwa pia na klabu ya AC Milan.
Nyota huyo anatajwa na gazeti hilo ambalo ni maarufu kwa uandishi wa habari za michezo kwamba usajili wake wa kutua Chelsea anauona ulikuwa wa makosa kwake huku kwa sasa akitajwa kutaka kuondoka klabuni hapo akitakiwa na klabu za nchini Italia, Juventus pamoja na AC Milan.
Klabu ya Juventus ambayo kabla aliwai kuichezea inatajwa kuwa tayari kumruhusu mshambuliaji wake Gonzalo Higuain ili atue Chelsea wao wamnase tena Morata.
Wakati kwa upande wa AC Milan wao wanatumikia adhabu ya usawa katika matumizi ya pesa (Financial Fair Play) na wanatajwa kumtaka Morata ingawa wanaweza wasiifate Chelsea katika dirisha hili kubwa la usajili. Wakaifata baadae.
No comments:
Post a Comment