Hazard azungumzia Chelsea kushindwa kushiriki Uefa kwa msimu ujao - Darajani 1905

Hazard azungumzia Chelsea kushindwa kushiriki Uefa kwa msimu ujao

Share This

Chelsea imeshindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao mara baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tano kwenye ligi kuu Uingereza, nafasi ambayo inainyima tiketi ya kufudhu kucheza michuano hiyo ambayo ili klabu ifudhu basi inalazimika kumaliza ndani ya klabu nne za juu ambayo hiyo ni kwa zile ligi zilizochaguliwa.

Kushindwa kwa klabu hiyo kufudhu kucheza michuano hiyo halionekani kuwa tatizo kwa nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambapo kwenye mahojiano aliyofanya amesema hiyo ni nafasi nzuri kwao kushinda taji kubwa kama ilivyotokea kwenye msimu wa kwanza wa kocha Antonio Conte klabuni hapo ambapo Chelsea ilitwaa taji la ligi kuu huku ikiwa haishiriki michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya.

"Msimu uliopita hatukuwa kwenye ushiriki wa klabu bingwa, kama itakavyokua msimu ujao lakini tulifanikiwa kutwaa ligi kuu ambapo hilo linaweza kutokea kwa msimu ujao. Kushindwa kushinda taji moja kunatufanya tupambane kushinda taji lengine. Na hiyo ndo sababu inayotufanya tuipende Chelsea" alisema nyota huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo ataiongoza kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi.

Badala ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya klabu ya Chelsea imefudhu kushiriki michuano ya ligi ya Ulaya (Europa League) ambapo mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ilikuwa msimu wa 2012-2013 ambapo waliibuka mabingwa wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment