Gary Cahill aiongoza vyema Uingereza, na matukio kibao ya kimataifa - Darajani 1905

Gary Cahill aiongoza vyema Uingereza, na matukio kibao ya kimataifa

Share This

Siku ya jana kulichezeka michezo ya kirafiki kwa timu za  taifa ambazo zinajiandaa kucheza michuano ya kombe la dunia itakayoanza mwezi Juni mwaka huu uko nchini Urusi.
 
Hapa nakuletea habari kuhusu nyota wa Chelsea waliocheza kwenye baadhi ya michezo hiyo.

Uingereza 2-1 Nigeria
Uingereza:
Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill aliliongoza vyema taifa lake la Uingereza kupata ushindi huo huku akifunga goli la kwanza huku goli la pili kwa timu hiyo likifungwa na nahodha wa timu hiyo, Harry Kane. Mara baada ya mchezo huo kuisha, Cahill alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo akiiongoza vyema timu yake haswa kwenye safu ya ulinzi. Nyota mwengine wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek aliichezea timu hiyo akiingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 64.
Nigeria; Kwa upande wa Nigeria, kikosi chake kiliundwa na winga wa Chelsea, Victor Moses huku mchezaji wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel akirejea tena nchini Uingereza tangu aachane na klabu hiyo na kujiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini China. Ola Aina alikosa nafasi ya kucheza kwenye mchezo huu huku mwenzake Keneth Omeruo ambaye naye ni mchezaji wa Chelsea akiingia kwenye mchezo huo kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 64.

Austria 2-1 Ujerumani
Ujerumani: Nyota mwengine wa Chelsea aliyesajiliwa akitokea nchini Italia na kufanikiwa kutengeneza taswira mpya klabuni Chelsea, Antonio Rudiger aliiongoza timu yake ya Ujerumani ikipoteza mbele ya timu ya Austria ambao kijiografia na kihistoria wa nchi hizo zina uhusiano mkubwa.

Sweden 0-0 Denmark
Denmark; Nyota mwengine wa Chelsea ambaye alishinda tunzo ya mchezaji bora chipukizi klabuni Chelsea, Andreas Christensen aliiongoza vyema timu yake ya Denmark kuondoka na suluhu ya bila kufungana dhidi ya Sweden waliokuwa nyumbani.

Ubelgiji 0-0 Ureno
Ubelgiji; Eden Hazard na Thibaut Courtois walikuwepo uwanjani wakiiongoza timu yao ya Ubelgiji kucheza dhidi ya timu ya mlinda mlango nambari tatu wa Chelsea, Eduardo ambaye kwa sasa hajaungana na timu hiyo na mchezo kuisha kwa suluhu ya bila kufungana huku Michy Batshuayi akikosa nafasi ya kucheza mchezo huo.

Michezo mingine itakayochezwa hii leo ni pamoja na Brazil yenye nyota wa Chelsea, Willian itakapokuwa uwanjani kucheza dhidi ya Croatia wakati mchezo mwengine utawahusisha Hispania yenye Cesar Azpilicueta itakayocheza dhidi ya Switzerland.

No comments:

Post a Comment