Roman Abramovich aipa mitihani mizito Chelsea - Darajani 1905

Roman Abramovich aipa mitihani mizito Chelsea

Share This

Jana kulitolewa taarifa kupitia mtandao maalumu wa Chelsea kuhusu kusitishwa kwa mpango wa upanuzi wa uwanja wa klabu hiyo, uwanja wa Stamford Bridge ambao ulitakiwa kuigharimu klabu hiyo kiasi cha zaidi ya paundi milioni 500.

Kusitishwa kwa mpango wa upanuzi huo kunatajwa haswa kusababishwa kwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kukosa kibali cha kuishi nchini Uingereza ambapo kibali hicho kilimalizika mwezi Aprili mwaka huu na tayari mmiliki huyo ameshahamishia makazi yake nchini Uingereza huku kukiwa na wasiwasi wa kuachana na mpango wa kuomba kibali kingine cha kuishi tena nchini Uingereza.

Kuondoka kwa tajiri huyo kunaelezwa na moja ya viongozi wa zamani wa Chelsea, Trevor Birch kuwa ni moja ya sababu zitakazoifanya Chelsea isiwe na mwenendo mzuri huku kukiwa sababu pia ya kuondoka kwa nyota Eden Hazard ambaye amekuwa akifukuziwa na Real Madrid huku pia kocha wake wa sasa Antonio Conte akitajwa kuondoka.

"No Stadium, no manager, no star player if Hazard will join Real Madrid" ndiyo kauli ya kiongozi huyo wa zamani ambaye aliwai kuwa mwanasoka nchini Uingereza akimaanisha kuondoka kwa Roman Abramovich kutaiacha Chelsea isitishe mpango wake wa upanuzi wa uwanja, kutaifanya isiwe na kocha mwenye ubora huku kocha wa sasa, Antonio Conte akitajwa kuondoka wakati pia itamkosa mchezaji nyota, Eden Hazard ambaye labda anaweza akatimkia Real Madrid.

Birch alisema pia alitambua kabisa kwamba kutokana na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich mwenye utajiri wa paundi bilioni 9.6 kukosa kibali cha kuishi Uingereza basi ingekuwa ni sababu kubwa kwa klabu hiyo kusitisha upanuzi huo ambao bajeti yake inatajwa kufikia paundi bilioni 1.

No comments:

Post a Comment