Katika nusu fainali ya kombe la FA kati ya Chelsea ilipomenyana dhidi ya Southampton, nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva alifanyiwa mabadiliko ambapo mara baada ya kupumzishwa alipitiliza na kupitia mlango wa kuingilia akionekana hakupendezwa kwa kupumzishwa kwake.
Tukio lilizua mjadala na moja kwenye mahojiano aliyofanyiwa nyota huyo raia wa Brazil aliulizwa kuhusu mahusiano yake na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambapo nyota huyo alicheka na kusema swali hilo atalijibu siku nyengine. Nadhani unakumbuka maana nilikuletea habari hii.
Hatimaye nyota huyo amefunguka juu ya nafasi yake kikosini huku akianza kwenye mchezo mmoja tu kati ya michezo mitano iliyopita wakati Chelsea ilipokuwa uwanjani.
"Nimekuwa ninafurahishwa na kiwango changu kwa msimu mzima, nimecheza vizuri na kwenye ubora mkubwa na mara zote nimekuwa nikijaribu kufanya juhudi kubwa. Muda mwengine kukaa benchi ni jambo linaloumiza lakini nimekuwa nikiheshimu maamuzi ya kocha."
"Sina mengi zaidi ya kusema kuhusu klabu yangu kwa sababu nahitaji kutazamia na kujihusisha haswa kuhusu timu yangu ya taifa kuelekea kombe la dunia" alisema winga huyo mwenye miaka 29.
Nyota huyo ambaye alishinda tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wa Chelsea huku akishinda pia tunzo ya goli bora la mwaka huku kukihusishwa kwamba nyota ataendelea kusalia klabuni Chelsea endapo klabu hiyo itaachana na kocha Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment