Davide Zappacosta anaiongoza vyema timu yake ya taifa ya Italia kutoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi huku nyota huyo wa Chelsea akicheza kwa dakika tisini.
Kocha Roberto Mancini amempa nafasi hiyo nyota huyo anayecheza kama mlinzi wa kulia au winga wa upande huo katika mchezo huo wa kirafiki ambao uliisha kwa sare hiyo huku mshambuliaji Simone Zaza akiifungia goli timu ya Italia.
Timu hiyo ya Italia haikupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa mwaka huu itakayoanza tarehe 17-Juni huko nchini Urusi.
Siku ya leo kutakuwa na michezo mingine ya kirafiki kwa timu za taifa ambayo haitoshirikisha nyota wa Chelsea.
No comments:
Post a Comment